Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Lebanon limeanza kuchukua udhibiti wa eneo la Zawtar al-Gharbiyeh kusini mwa nchi hiyo baada ya vikosi vya Israel kujiondoa, hatua inayotekelezwa chini ya mpango ulioratibiwa na Marekani.

Wakaazi waliokimbia makazi yao walikusanyika pembezoni mwa eneo hilo siku ya Jumanne wakisubiri ruhusa kutoka kwa jeshi la Lebanon kurejea nyumbani.

Mpango huo unatarajiwa kuona jeshi la Lebanon likikusanya silaha kutoka kwa kundi la Hezbollah katika baadhi ya maeneo ya kusini mwa nchi huku vikosi vya Israel vikiondoka hatua kwa hatua.

Wanajeshi wa Israeli wameanza kujiondoa Kusini mwa eneo kwa mujibu wa mpango unaoratibiwa na Marekani.
Wanajeshi wa Israeli wameanza kujiondoa Kusini mwa eneo kwa mujibu wa mpango unaoratibiwa na Marekani. REUTERS – Aziz Taher

Makabidhiano ya eneo hilo ni jaribio la kwanza la mpango ambao Lebanon ina matumaini utaisaidia kurejesha udhibiti wa sehemu ya kusini mwa nchi hiyo ambayo bado imeathiriwa na uwepo wa vikosi vya Israel.

Vijiji vingi katika eneo hilo vimeharibiwa, huku hospitali, vituo vya umeme na miundombinu ya maji ikiteketezwa. Maelfu ya wakaazi hawajarejea makwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *