Kulingana na takwimu kutoka nchi kadhaa za Afrika, zaidi ya raia 150,000 wameondoka Afrika Kusini kutokana na wimbi hili jipya la chuki dhidi ya wageni linaloikumba nchi hiyo, ambalo tayari limesababisha vifo vya watu wanne, kulingana na mamlaka ya Afrika Kusini.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Johannesburg, Valentin Hugues

Afrika Kusini, taifa lenye nguvu kiuchumi, linawavutia wageni wengi wanaotafuta maisha bora, lakini waandamanaji wanawalaumu kwa matatizo yote ya kijamii, ingawa wanawakilisha 5% tu ya idadi ya watu na ukosefu wa ajira unazidi 30%. Katika baadhi ya mashamba, kuondoka huku kwa watu wengi kunasababisha uhaba wa wafanyakazi.

Wakulima kadhaa wa Afrika Kusini wanaanza kutoa tahadhari, anaelezea Lloyd Hadebe, naibu mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (Afasa) huko KwaZulu-Natal, eneo lililoathiriwa zaidi na maandamano dhidi ya wahamiaji.

“Bado hatuna takwimu sahihi, kwani bado tunapima hali hiyo. Lakini tayari kuna uhaba wa wafanyakazi katika mashamba ya miwa, kwa mfano, kwa sababu hizi ni sekta zinazohitaji kazi ya mikono karibu kila siku,” anabainisha.

Uhamiaji, ufisadi, na mvutano unaozunguka soko la ajira

Hali hii inachochea mijadala mingi mikali. Baadhi wanawashutumu wakulima kwa kuajiri wahamiaji wasio na vibali halali ili kuwalipa mishahara midogo. Wengine wanashtumu shinikizo la kiuchumi na ugumu wa kupata vibali vya kisheria. Zaidi ya yote, hali hii inaonyesha mamlaka ya uhamiaji ya Afrika Kusini inayoshindwa kuwajibika katika majukumu yake na ambayo ufisadi umekithiri.

“Tutajaribu kushirikiana na serikali ili kuimarisha sheria zetu za uhamiaji, lakini pia kuhakikisha wanajitahidi kurekebisha hali ya wale wanaokidhi mahitaji ya hadhi ya kisheria. Hii ni kukomesha vipindi hivi virefu vya kusubiri kwa wale wanaohitaji kutatua masuala yao ya kiutawala,” Lloyd Hadebe anaelezea.

Vyama kadhaa vya wafanyakazi vya Afrika Kusini (Safatu na Cosatu, miongoni mwa vingine) vinaongeza kwamba “kukatishwa tamaa kwa jamii za wenyeji lazima kushughulikiwe kwa kurekebisha uchumi,” na si kwa kuwafanya wahamiaji “kuwa kama watu wa kubeba lawama kwa kushindwa huko ambapo hawahusiki.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *