Wakazi wa Makazi ya Wakimbizi Ulyankulu, Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wamehakikishiwa kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Mwadui, Kijiji cha Taba, Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, Japhael Lufungija amesema wakazi wa makazi hayo wana haki ya kupata mikopo hiyo kama wananchi wengine, mradi vikundi vyao vitimize vigezo na masharti yaliyowekwa. Amesisitiza wenye uhitaji kujiunga na vikundi vinavyotambulika ili waweze kunufaika na fursa hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Makazi ya Wakimbizi Ulyankulu, Jumanne Singani, amewahimiza wakazi kuchangia ujenzi wa jengo la huduma za mionzi katika Kituo cha Afya Ulyankulu, akieleza kuwa huduma hiyo bado haipatikani na ni muhimu katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wakazi wa Makazi ya Ulyankulu pamoja na viongozi wa Kijiji cha Taba.
(Feed generated with FetchRSS)