Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Benki ya Azania imezindua rasmi mradi mkubwa wa utoaji wa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo, utakaofanikisha ujenzi na uendeshaji wa vituo vidogo vya kuuza mafuta ya petroli na dizeli maeneo ya vijijini.
Hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya mafuta, kupunguza gharama zisizo za lazima kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba kwa wanufaika nane wa kwanza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi), Dkt. James Mataragio, ameema serikali imeamua kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi ili kumaliza changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata nishati hiyo.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)