Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa kutekeleza mashambulizi mapya dhidi ya ngome za kijeshi za Marekani nchini Kuwait na Bahrain, huku likitoa onyo kwa raia katika nchi zinazowapa hifadhi wanajeshi wa Marekani kuondoka mara moja na kuwa mbali kwa angalau mita 500 kutoka maeneo yanayotumiwa na wanajeshi hao.

Katika taarifa mbili tofauti siku ya Ijumaa, IRGC imesema mashambulizi hayo ya karibuni yalifanywa katika wimbi la 27 la Operesheni Nasr 2, ikiwa ni majibu kwa uchokozi unaoendelea wa Marekani dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikosi vya Iran vimevurumisha droni nzito za kisasa za mashambulizi dhidi ya Kambi ya Anga ya Ali Al Salem inayosimamiwa na Marekani nchini Kuwait, na kuharibu ghala kubwa la silaha kupitia milipuko ya mfululizo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Marekani imeficha kiwango halisi cha hasara zake katika medani ya mapambano katika kipindi cha vita vya miezi mitano, ikibainisha kuwa mamia ya wanajeshi wa Marekani wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Katika taarifa nyingine, IRGC imesema imekamilisha operesheni ya awali dhidi ya kituo cha data cha Amazon nchini Bahrain, ikikieleza kuwa ni kituo muhimu cha kijasusi kinachounga mkono jeshi la Marekani.

Aidha, IRGC imetangaza kulenga mnara wa udhibiti wa Kikosi cha Tano cha Jeshi la Majini la Marekani nchini Bahrain, na kusababishia uharibifu mkubwa.

Hayo yanajiri huku jeshi la Marekani likiendelea kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya Iran kwa usiku 13 mfululizo. Jeshi katili la Marekani linalenga maeneo ya kiraia yakiwemo madaraja na mitambo ya maji safi.

Vitendo hivyo haramu vya uchokozi vya Marekani dhidi ya Iran vimesababisha watu 55 kuuawa na wengine 645 kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo mapya yalianza upya baada ya Washington kuachana na ahadi zake chini ya Hati ya Maelewano ya Islamabad, ambayo ilikusudiwa kusitisha mapigano kufuatia vita vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran vilivyoanzishwa Februari 28. Usitishaji vita ulikubaliwa baada ya siku 40 kutokana na operesheni za kujibu za Iran na udhibiti wake juu ya Lango-Bahari la Hormuz.

IRGC imesisitiza kuwa wanajeshi wengi wa Marekani wameondoka katika kambi zao kwa kuhofia mashambulizi ya Iran na sasa wanaendesha shughuli zao wakiwa ndani ya majengo ya kiraia katika nchi zinazohifadhi vikosi vya Marekani.

IRGC imewaonya raia wote katika nchi ambazo zimeruhusi ardhi zao kutumiwa na jeshi vamizi la Marekani kuondoka mara moja na kuwa mbali kwa angalau mita 500 kutoka maeneo yanayotumiwa kwa siri na wanajeshi Marekani.

Pia IRGC imetoa wito kwa wananchi wa nchi za eneo kuripoti maeneo mapya yanayotumiwa na wanajeshi wavamizi wa Marekani kupitia akaunti rasmi ya Telegram ya Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya IRGC, @sepahnewsiradmin, au kupitia sehemu ya Contact katika tovuti ya Sepah News.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *