Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amelaani vikali shambulio la kijeshi lililofanywa na utawala wa Ukraine dhidi ya meli ya biashara ya Iran katika Bahari ya Caspian.

Sayyid Abbas Araqchi ametoa tamko hilo kali katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na mkuuuu wa Sera za Kigeni wa UUmoja wa Ulaya ambapo amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya tukio hilo na kuhakikisha wahusika pamoja na wanaounga mkono kitendo hicho cha uhalifu wanawajibishwa.

Katika mazuungumzo yao hayo ya simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi, na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, wamejadili pia matukio ya hivi karibuni katika ngazi ya kikanda na kimataifa.

Aidha katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilijadili hali ya Ghuba ya Uajemi na Mlango-Bahari wa Hormuz kufuatia hatua ya kujibu iliyochukuliwa na Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya mashambulizi ya Marekani. Wanadiplomasia hao wmeisisitiza umuhimu wa kuanzisha mipango ya kidiplomasia ili kudhibiti na kupunguza mvutano unaoendelea katika eneo hilo.

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali shambulio lililofanywa na utawala wa Ukraine dhidi ya meli ya biashara ya Iran katika Bahari ya Caspian alfajiri ya jana Jumamosi. Shambulio hilo lilisababisha mlipuko mkubwa katika meli hiyo, na kupelekea baharia mmoja kuuawa shahidi huku mwingine akijeruhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *