Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Iran ameliambia shirika la
habari la Reuters siku ya Jumapili kuwa itasitisha mashambulizi yake, mradi tu
Marekani nayo iendelee kusitisha mashambulizi yake, kulingana na afisa mmoja
mwandamiz.
Hatua hiyo imekuja baada ya
Marekani kusitisha kwa muda kampeni yake ya mashambulizi ya anga, kufuatia
washauri wa Rais Donald Trump kumweleza kuwa walikuwa wakikabiliwa na wasiwasi
kuhusu kupungua kwa akiba ya silaha za Marekani.
Baada ya usiku 13 mfululizo
wa mashambulizi makali ya anga ya Marekani dhidi ya Iran, Wizara ya Ulinzi ya
Marekani ilisisitisha operesheni hiyo mwishoni mwa Ijumaa.
Hakukuwa na mashambulizi
yoyote ya Marekani yaliyoripotiwa Jumamosi wala Jumapili.
Kwa upande wake, Iran,
ambayo ilikuwa ikijibu kila usiku wa mashambulizi ya Marekani kwa kushambulia
nchi jirani zinazohifadhi kambi za kijeshi za Marekani, pia haijafanya
mashambulizi yoyote kwa siku mbili zilizopita hadi sasa.
Afisa huyo wa Iran, ambaye alizungumza na shirika la
habari la Reuters kwa sharti la kutotajwa jina, alisema msimamo wa Tehran
unaendelea kuwa “shambulio kwa shambulio.” Alieleza kuwa, “Iwapo
mashambulizi yatasitishwa, Iran pia itasitisha operesheni zake. Ujumbe huo
tayari umefikishwa kwa Marekani.”
Kwa upande mwingine, Balozi wa Marekani katika Umoja wa
Mataifa, Mike Waltz, aliviambia kipindi cha Fox News Sunday pamoja na vyombo
vingine vya habari vya Marekani kuwa Rais Donald Trump aliamua kusitisha kwa
muda mashambulizi ya Marekani ili kutoa nafasi zaidi kwa juhudi za
kidiplomasia.
Akizungumza kuhusu uamuzi wa Rais Donald Trump, Balozi wa
Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, alisema:
“Antoa fursa kwa mazungumzo yaendelee; anatoa muda
kidogo ili yaweze kusonga mbele.”
Maafisa wa jeshi la Marekani katika siku za karibuni
wameonya kuwa mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita, yaliyolenga kuzuia vitisho vya Iran dhidi ya usafirishaji wa meli
katika Mlango-Bahari wa Hormuz—njia ya maji ambayo imesababisha mvutano
katika vita hivyo—yalikuwa yamekaribia kumaliza maeneo lengwa yaliyokuwa
yamechaguliwa mapema kwa ajili ya kushambuliwa, kwa mujibu wa afisa mmoja wa
Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina.
Soma Zaidi: