
KOCHA wa Utimamu wa Mwili, Ikra Amour Khamis ‘Ikidas’ amejiunga na timu ya Villa iliyopo ligi daraja la kwanza kanda ya Unguja iliyopanda daraja msimu huu.
Kabla ya kujiunga na kikosi hicho, Kocha Ikidas alikuwa anafanya kazi na timu ya Magomeni City inayoshiriki igi daraja la pili Mkoa wa Mjini Unguja.
Baada ya kusaini timu hiyo, Kocha huyo amesema anashuru kupata nafasi hiyo kwani wapo wengi lakini uongozi wa timu ya Villa walimuona yeye anafaa.
Amesema, atafanya kazi kwa biidi na achohitaji zaidi ni ushirikiano kutoka kwa uongozi na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kufanyakazi kwa pamoja.
“Nimepiga hatua moja mbele hili ni jambo zuri awali nilikuwa daraja la pili sasa la kwanza nimepata moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii,” amesema
Amesema, Malengo yake anahitaji kufika mbali zaidi ya hapo kwa kufanya kazi na klabu kubwa za ndani na nje ya Tanzania ndiyo maana anapambana kufanikisha hilo.