SHINYANGA: BAADHI ya wakazi wa kata ya Ubagwe na Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameeleza historia kabla ya kujengwa daraja la Ubagwe lenye urefu wa mita 60 eneo hilo kwamba walikuwa wakijipatia kipato kipindi cha masika kwa kuwavusha watu kwa Sh 5,000 na pikipiki Sh 1,000.

Jumanne Lyantemi mmoja wa mkazi wa maeneo hayo ameeleza mbele ya Naibu Waziri wa ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ambapo alieleza eneo hilo kulikuwa na mto mdogo kadri mvua zilipokuwa zikinyesha ulikuwa ukitanuka na kuwafanya watu kushindwa kuvuka.

Lyantemi amesema wamejenga historia ndani ya kata hizo mbili ilifikia hatua ya kununua mtumbwi kwaajili ya kuwavusha watu na walikuwa wakikaa watu wanne wanne au pikipiki mbili nakupelekea kuona inawapa faida na usafiri kuuboresha zaidi nakufanya watu wakae watatu watatu.

“Tumeziokoa familia nyingi sana zilizokuwa zikivuka tunashukuru serikali kutujengea daraja hili ambalo kwa sasa changamoto kama awali hakuna hata pesa tuliyokuwa tukiipata kwenye eneo hili sasa hakuna kila mmoja haamini uwepo wa daraja na wengine wamekuwa wakija kupigia picha za harusi hapa,”amesema Lyantemi.

Pia mkazi wa Ulowa Hassan Masele amesema daraja hili lilikuwa dogo mvua ikinyesha kubwa lilikuwa linajaa maji kusafirisha mgonjwa ilikuwa ikiwalazimu kuzunguka umbali mrefu na wengine walikuwa wakifika wamechoka nakupoteza maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *