Jeshi la polisi mkoani Morogoro limeanza uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mkazi wa mkoa huo aliyefahamika kwa jina la Gidion Ebenezeri Mbwambo (34) ambaye amekutwa amekufa kwenye nyumba la kulala wageni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema kifo hicho kimetokea leo Januari 27, 2026 katika nyumba ya kulala wageni ‘Kisanga’ iliyopo mtaa wa Nguzo kata ya Mazimbu.

Kamanda Mkama ameongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu amejiua kwa kujikata kooni.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *