#HABARI: Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani Songwe umeanza rasmi kazi ya upanuzi wa miundombinu ya barabara katika mpaka wa Tunduma unaounganisha Tanzania na Zambia.

Zoezi hilo limehusisha uvunjaji wa sehemu ya ukuta wa kituo cha forodha kinachosimamiwa na TRA pamoja na kuwahamisha wafanyabiashara wadogo waliokuwa kwenye hifadhi ya barabara, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bw. Jabir Makame, aliyoyatoa Januari 26, 2026, ili kuondoa msongamano wa magari mpakani hapo.

Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe, Mhandisi Silvan Mloka, ameeleza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita na utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kasi ya magari makubwa kuvuka mpaka huo. Hatua hii inalenga kuboresha mazingira ya kibiashara na ufanisi wa kituo cha forodha cha Tunduma, ambacho ni kiungo muhimu cha usafirishaji wa mizigo kati ya Tanzania na nchi za Kusini mwa Afrika.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *