#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mbeya, Bw. Justice Kijazi, amewapiga marufuku watumishi wa halmashauri hiyo kufunga maduka ya wafanyabiashara wanapochelewa au kukiuka taratibu za ulipaji kodi.
Badala yake, amewaagiza watumishi hao kutumia njia za kidiplomasia na kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kutengeneza mazingira rafiki yatakayochochea ulipaji wa kodi kwa hiari na uelewa bila kuathiri shughuli zao za kiuchumi.
Agizo hilo limetolewa katika kikao maalum kilichowakutanisha viongozi wa jiji na wafanyabiashara kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazozorotesha biashara jijini humo.
Bw. Kijazi amesisitiza kuwa kufunga maduka kunarudisha nyuma maendeleo, hivyo ni vyema kutumia majadiliano ili kumpa mfanyabiashara nafasi ya kuendelea na uzalishaji huku akitekeleza wajibu wake wa kisheria kwa serikali.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.