#HABARI: Serikali imeweka wazi kuwa haina mpango wa kuweka sheria kali inayowalazimisha watoto kuwahudumia wazazi wao wasiojiweza, badala yake inategemea misingi ya kifamilia na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Tarimba Abbas, aliyehoji haja ya kuwepo kwa takwa la kisheria kwa jambo hilo.

Mhe. Mahundi amefafanua kuwa utunzaji wa wazee ni sehemu ya mila, desturi, na mshikamano wa Kitanzania ambao unapaswa kuendelezwa ndani ya ngazi ya familia.

Ili kuimarisha hali hiyo, Serikali imefanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Wazee (2024) ambayo inasisitiza wajibu wa jamii katika kuwahudumia wazee huku ikiboresha mifumo ya kisheria itakayolinda ustawi wa wazee na wale wanaowatunza.

Kwa sasa, Serikali inaendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuboresha sheria zinazohusu wazee nchini.

Lengo kuu ni kuendelea kuhamasisha maadili ya uwajibikaji ndani ya familia na kuimarisha mifumo ya kijamii itakayohakikisha wazee wanaishi kwa heshima na kupata matunzo stahiki bila kulazimishwa kwa shinikizo la kisheria pekee.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *