#HABARI: Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB) imewataka wananchi, wadau na wataalamu wa mipango miji nchini kuhakikisha utekelezaji wa shughuli zote za mipangomiji unazingatia kikamilifu sheria, kanuni na miongozo ili kuondoa migogoro mbalimbali ya ardhi katika jamii.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB), TP. Martha J. Mkupasi kupitia taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa kazi za mipangomiji zinazoendelea kutekelezwa nchini ambapo amebainisha kuwa uzingatiaji wa sheria na kanuni unasaidia kuepusha migogoro katika jamii hivyo amewasihi wananchi kuwa makini wanapohitaji huduma za mipangomiji .

“Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji inapenda kuujulisha umma kuwa, shughuli za mipangomiji zinapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya sheria, kanuni na miongozo. Kifungu cha 22, 23, 24 na 25A cha Sheria ya Usajili wa wataalam wa Mipangomiji Sura 426 vinazuia mtu au kampuni isiyosajiliwa na Bodi kujihusisha na kazi za mipangomiji.

Aidha Kaimu Msajili huyo amewataka wote wanaokiuka sheria za mipangomiji kuacha mara moja vitendo hivyo,huku akisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kutekeleza kazi za mipangomiji kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *