
Moshi. Wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vinywaji baridi, Coca Cola, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamefanikiwa kutoa zaidi ya kreti 3,240 za soda kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wa Kanda ya Kaskazini.
Kreti hizo za soda zimetolewa kupitia droo ya Coca Cola VIP Club, ambayo imeendeshwa katika Kiwanda hicho ambacho kipo katika Manispaa ya Moshi, ikilenga kuimarisha biashara na kusaidia wafanyabiashara katika kukuza mitaji yao.
Wakizungumza wafanyabiashara hao, wamesema zawadi hiyo itawasaidia kukuza mitaji yao pamoja na vipato vyao vya Kila siku.
Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara walioshinda katika droo hiyo kutokea Mkoani Arusha, Dorine Mwaisango, amesema kupata kwake zawadi ya kreti 50 za soda itamasaidia kuongeza na kukuza mtaji wa biashara yake.
“Zawadi hii niliyoipata itanisaidia kuongeza mtaji wangu, kreti hizi 50 za soda nitaitumia kutengeneza faida, na kwa namna moja au nyingine, itaniongezea kipato na kuboresha biashara yangu.”amesema mfanyabiashara huyo
Mfanyabiashara mwingine, Florida Evarist, amekishukuru Kiwanda hicho kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha na kuwapongeza mtaji wafanyabiashara.
“Mchezo huu ulikuwa mzuri, na nashukuru kwa kushinda kreti zangu 30 za soda, hata wale ambao hawakushinda, wasikate tamaa, waendelee kuweka bidii zaidi ili kupata matokeo mazuri katika biashara zao.”amsema mfanyabiashara huyo
Ernest Barabara, mshiriki wa mashindano haya, amesema kuwa mashindano hayo yamekuwa na manufaa makubwa na kwamba yamekuwa yakiwasaidia kuinua biashara zao.
“Mashindano haya yamekuwa na manufaa kwangu, nilichopata si kidogo, ni kizuri na nitakitumia kuongeza kipato changu.”amsema mshindi wa mashindano hayo
Akizungumza, Mkuu maauzo na masoko, wa Kiwanda hicho, Christopher Loiruk amesema kupitia droo hiyo wameweza kuwainua wafanyabiashara mbalimbali wa Kanda ya Kaskazini kwa kuongeza mtaji wa biashara zao.
“Leo ni siku maalumu ya droo ya Coca Cola VIP Club, ambapo tumewasajili wateja wetu maalumu, wateja hawa wamekuwa wakitusapoti katika biashara zao na kusaidia kueneza bidhaa zetu. Lengo letu ni kuboresha biashara zao na kuwasaidia kuongeza mitaji yao.
Amesema “Tunatoa zawadi mbalimbali kama magari, pikipiki, na vinywaji baridi, hii ni kwa lengo la kuwahamasisha na kuendelea kuongeza bidii katika biashara zao,”
Amesema katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro kutakuwa na washindi 54 ambao watajishindia kreti 30, 50 na 100 ambapo katika droo hiyo jumla ya kreti za soda 3,240 zitatolewa kwa washindi.