#HABARI: Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala – WRRB kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo katika vyama vya ushirika, kuongeza thamani ya mazao pamoja na kuimarisha uwazi kwa wananchi, ili kuwafanya wajione kuwa sehemu ya mchakato wa maendeleo na hivyo kupunguza malalamiko.

Naibu Waziri ameyasema hayo jijini Dodoma baada ya kufanya ziara ya kikazi na kutembelea Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala ambapo amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuboresha mfumo wa stakabadhi za ghala na kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wakulima na wadau wa sekta ya kilimo.

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala – WRRB Asangye Bangu, amesema bodi hiyo inaelekea kuadhimisha miaka 20 ya mchango wake katika kuwawezesha wakulima, wawekaji wa amana pamoja na wadau mbalimbali kwa ajili ya kujenga mustakabali endelevu.

Amesema Maadhimisho haya ni ushuhuda wa safari yao ya miaka 20 ya kushirikiana na wakulima, wawekaji wa amana na wadau weo ambapo amesema wamejikita katika kujenga mifumo endelevu ya kifedha kwa maendeleo ya sasa na ya baadaye.

Uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB unatarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 8 hadi 10, 2026, ambapo kutakuwa na maonyesho, mijadala ya maendeleo, pamoja na utoaji wa elimu kuhusu fursa za kifedha na uwekezaji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *