#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ametembelea chanzo cha maji cha Mto Ungwasi ili kutafuta suluhisho la kudumu la adha ya maji wilayani humo.
Katika ziara hiyo, Profesa Mkenda aliambatana na wataalamu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo pamoja na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo.
Lengo kuu la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua maendeleo ya mradi huo uliopo kwenye eneo lenye miinuko na vikwazo vya kijiografia ili kuona hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma hiyo kwa jamii.
Profesa Mkenda alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali, changamoto ya maji bado ndiyo inayowagusa wananchi wengi wa Rombo, hivyo uwekezaji zaidi unahitajika.
Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wataalamu na wadau wa maendeleo kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.
Viongozi na wataalamu walioambatana naye wameahidi kusimamia mradi huo kwa ukaribu ili kuondoa kabisa kero ya maji na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii jimboni humo.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA >>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)