
Nchini Sudan, mvutano umehamia katika jimbo jipya la kusini, Blue Nile, linalopakana na Ethiopia na Sudan Kusini. Kwa wiki iliyopita, eneo hili limekuwa uwanja mpya wa mapigano kati ya jeshi la serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), wanaoungwa mkono katika jimbo hili na kundi la waasi la SPM-N la Abdelaziz el-Hilu. Wakiwa wamejikita kwenye vita vya Kordofan na Darfur, RSF na washirika wao walishambulia ngome kadhaa za jeshi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi lilitangaza wiki hii kwamba limechukua tena maeneo yake, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo kando ya mpaka wa Ethiopia.
Mapigano haya mapya yaliandaliwa tangua zamani. Jeshi la Sudan liliionya Addis Ababa, likiishutumu kwa kutoa silaha na risasi kwa wanamgambo na waasi, pamoja na kuwafunza wapiganaji katika kambi linalopatikana katika eneo lake kupigana vita dhidi ya Sudan. Jeshi limetuma Kitengo cha 4 cha wanajeshi wa nchi kavu kwenda Damazin, mji mkuu wa Blue Nile, kama kikosi cha usaidizi na linaendelea kuimarisha ngome zake katika eneo hilo.
Mapigano haya huko Blue Nile yanakuja huku pande mbili zinazopigana zikijaribu kudhibiti maeneo ya kimkakati na njia panda muhimu katika maeneo ya Darfur na Kordofan, magharibi na kusini mwa nchi, mtawalia. Kulingana na baadhi ya wataalamu wa kijeshi, wanamgambo wa RSF na wapiganaji wa kundi la waasi la SPM-N la Abdelaziz al-Hilu huko Blue Nile haziwezi kutenganishwa na shughuli zinazoendelea huko Darfur na Kordofan.
Vikosi vya Sudan (SRF) vinakabiliwa na shinikizo linaloongezeka katika, vita. Ili kupunguza shinikizo hili na kugeuza umakini kutoka Darfur na Kordofan, kwa hivyo wanafungua “njia za pembeni,” kulingana na chanzo. Mto Blue Nile una nafasi nyeti ya kimkakati na faida kubwa. Ni njia ya biashara na magendo. Kudhibiti kunahusisha masuala ambayo yanaenea zaidi ya Sudan na kuathiri eneo lote.
Ushiriki wa Ethiopia
Abdelaziz al-Hilu amekuwa akipigana na serikali tangu mwaka 2011. Anadai uhuru wa Kordofan ya Kati na pia kwa Blue Nile. Jeshi la Sudan linaishutumu Ethiopia kwa kumruhusu kuanzisha kambi katika ardhi yake.
Pia linaishutumu Sudan Kusini kwa kuwahifadhi wapiganaji wa RSF. Hali hii inafanya uwezekano wa kuongezeka kwa mashambulizi yoyote ya kijeshi katika nchi hizo mbili jirani, ambazo hali zao za kisiasa na kiusalama ni tete.