#HABARI: Waziri wa Afya nchini Tanzania Mhe. Mohamed Mchengerwa Jumatatu Februari 02, 2026, anatarajiwa kuwa na ziara ya Kikazi kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam kukagua utekelezaji wa maagizo yake pamoja na kuzindua mradi wa PET/ CT Scan wa Taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Januari 30, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road Dkt. Diwani Msemo amesema utekelezaji wa Mradi huo wa PET/CT Scan ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia na kutoa zaidi ya Bilioni 18 ili kusimikwa kwa mtambo huo utakaoondoa adha ya Wagonjwa kusafirishwa kwenda India kufuata huduma hiyo ya vipimo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.