#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikiria Filbert Philimon (23) mwanachuo wa Chuo kikuu cha St. John’s aliyehusika katika tukio la kuchoma chumba moto na kusababisha vifo vya watu wawili (Rebeka James na Felister Peter) huko mtaa wa Kikuyu Dodoma mjini Juni 7, 2026 saa nane usiku.
Baada ya tukio hilo la uhalifu kutendeka, Jeshi la Polisi Dodoma lilifanya uchunguzi wa haraka na wenye umahiri wa hali ya juu uliofanikisha kubainisha kuwa tukio hili limetendwa na mtuhumiwa huyu. Hivyo mnamo Juni 13, 2026 ndipo alipokamatwa huko stendi ya mabasi ya Magufuli Dar es Salaam akiwa katika harakati za kuukimbia mkono wa sheria.
Aidha, mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo Kwa kutumia mafuta ya petrol lita mbili sababu kubwa ikiwa ni wivu wa mapenzi baada ya kuachwa na mpenzi wake marehemu Felister Peter Francis ambaye alimpata mwanaume mwingine.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linatoa wito na kuwaasa wananchi na wanavyuo wa elimu
ya juu kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu kama ilivyo katika tukio hili. Nawasihi wanavyuo kuendelea na masomo yao ipasavyo huku wakizingati sheria za vyuo na za nchi wajiepushe na vitendo visivyozingatia maadili mema ya Mtanzania, matumizi ya dawa za kulevya, matumizi ya mitandao ya kijamii katika kupanga na kushiriki uhalifu. Pia watafute msaada wa kisaikolojia na kutembelea washauri nasihi ili kukabiliana na msongo wa mawazo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)