Katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake Stephane Dujarric, Guterres amesema vikosi vya serikali na vya upinzani vinapaswa kuchukua hatua za mara moja na maamuzi ya kusitisha shughuli zote za kijeshi pamoja na kupunguza vurugu hizo kupitia mazungumzo jumuishi.

Matamshi yake yanakuja baada ya jeshi la nchi hiyo kuwaamuru raia na wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na mashirika yote ya misaada kuondoka katika kaunti tatu kwenye Jimbo la Jonglei kabla ya kufanyika kwa operesheni dhidi ya vikosi vya upinzani katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *