
Maswali mengi yanaulizwa kuhusu athari za ongezeko la joto duniani kwa malaria. Tafiti kadhaa zinaelezea ongezeko la eneo lililoambukizwa huku mbu wanaoeneza vimelea hivyo wakichukua fursa ya hali ya hewa ya joto kusambaa hadi maeneo ambayo hawapo kwa sasa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Utafiti wa kisayansi uliochapishwa wiki hii katika jarida la Nature unaonyesha kwamba athari za ugonjwa huo pia zitazidi kuwa mbaya zaidi katika maeneo ambayo tayari mbu hao yuko na kusababisha mamia ya maelfu ya vifo vipya barani Afrika katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Bara la Afrika tayari linakabiliwa na 95% ya visa vya malaria duniani. Kwa bahati mbaya, mzigo huu utaongezeka katika siku zijazo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, hata kama ahadi za kimataifa za kuupunguza zitatimizwa. Waandishi wa utafiti huu wa kimataifa uliochapishwa katika jarida la Nature wanatarajia visa vipya milioni 123 na vifo vipya 500,000 ifikapo mwaka wa 2050.
Kuongezeka visa vya maambukizi
Sio sana kupitia upanuzi wa kijiografia wa ugonjwa huo, bali kupitia kuongezeka kwa kasi katika maeneo ambayo tayari mbu hao wamesambaa. Ili kufikia hitimisho hili, wanasayansi wametathmini athari za “kiikolojia” za mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile athari za mabadiliko ya hali ya hewa na mvua kwa idadi ya mbu, na athari za “usumbufu” wa matukio mabaya ya hali ya hewa.
Ustahimilivu
Mafuriko, dhoruba, na vimbunga, vinavyotokea mara kwa mara na vikali zaidi katika ulimwengu wenye joto, vitazuia utendakazi mzuri wa programu za kuzuia na miundombinu ya afya. Jambo hili la mwisho ndilo linalosababisha ongezeko kubwa la visa vinavyotarajiwa. Kwa hivyo, waandishi wanahitimisha kwamba hapa ndipo kazi ya kipaumbele inapaswa kuzingatiwa, haswa kwa kufanya mifumo ya afya ya jamii iweze kustahimili usumbufu kama huo.