
Jeshi la Marekani limesema kuwa halitavumilia mienendo “isiyo salama” kama vile ndege kuruka juu ya meli za kivita za Marekani, au boti ndogo za kasi za Iran kukaribia meli za Marekani katika mazoezi hayo ambayo yamepangwa kufanyika kesho.Taarifa yake iliendelea kuonya kuwa Jeshi la Marekani lina kikosi chenye mafunzo ya hali ya juu na uwezo mkubwa zaidi duniani, na litaendelea kufanya kazi kwa viwango vya juu zaidi vya taaluma na kufuata kanuni za kimataifa na kuongeza kuwa IRGC ya Iran nayo inapaswa kufanya vivyo hivyo. Ujia wa Bahari wa Hormuz, njia ya maji yenye upana wa kilomita 55 kati ya Iranna Oman, ni moja ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta kwenda nje ya nchi.