m

Chanzo cha picha, Saronic

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 4

Jeshi la Marekani linasema lilitumia chombo cha majini kisicho na muelekezi kuwaokoa wafanyakazi wawili kutoka kwa helikopta ya Jeshi la Marekani iliyoanguka katika pwani ya Oman mapema wiki hii.

Hiki ni mara ya kwanza ambapo chombo kisicho na muelekezi kimetumika kutekeleza shughuli ya uokoaji.

Kwa mujibu wa Rais Donald Trump, helikopta ya Apache ilidunguliwa na Iran karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz, njia kuu ya majini ambayo imefungwa tangu kuanza kwa vita vya Iran.

Wanajeshi hao wawili “waliokolewa ndani ya takriban saa mbili na wako katika hali nzuri,” Kamandi kuu ya Jeshi la Marekani (Centcom) iliripoti.

BBC Verify imechanganua taarifa zilizopo kuhusu chombo hiki kisicho na muelekezi na jinsi operesheni hiyo ya uokoaji ilivyofanyika.

Droni ya majini ya Marekani ikoje?

Centcom imethibitisha kuwa Corsair, chombo cha majini kisicho na muelekezi iliyotengenezwa na kampuni ya droni ya wanamaji ya Texas, ilitumika katika uokoaji.

Ina urefu wa mita 7.3, uwezo wa kubeba mzigo wa takriban kilo 450 na inaweza kusafiri kwa zaidi ya knots 35 (kama kilomita 65 kwa saa), kulingana na tovuti ya kampuni hiyo.

“Corsair inakaribia ukubwa wa mashua ya wavuvi. Imeundwa kubeba mizigo na pengine ina nafasi ya watu watatu hadi wanne,” anasema Bryan Clark, mtaalamu wa ndege zisizo na rubani katika Taasisi ya Hudson.