Miongoni mwa uporaji uliotajwa ni kulipa dola bilioni 1.7 kwa makampuni yanayohusishwa na Makamu wa Rais Benjamin Bol Mel kwa ujenzi wa barabara ambayo haijawahi kufanyiwa kazi yoyote.

Kulingana na ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, malipo hayo yalikuwa sehemu ya ufisadi mkubwa katika taifa hilo maskini.

Ripoti imetaja pia kiwango cha fedha kilichotengewa matibabu ya rais ambacho kimezidi bajeti ya afya ya nchi nzima.

Kwenye jibu rasmi kwa tume ya Umoja wa Mataifa, waziri wa sheria Joseph Geng alisema ripoti hiyo ilijikita kwenye takwimu ambazo haziendani na data kamili za serikali.

Amesema matatizo ya kiuchumi ya Sudan Kusini yamesababishwa na machafuko, mabadiliko ya tabia nchi na kushuka kwa bei ya mafuta yake.

Hii si mara ya kwanza kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwatuhumu wanasiasa wa Sudan Kusini kuwa mafisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *