Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea riwaya inayoitwa “Uzi wa Buibui” iliyoandikwa na Akutagawa Ryunosuke. Hadithi hii inagusia kisa kilichotokea baada ya Buddha Shakyamuni kuchungulia jehanamu.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!