Taasisi ya ushauri ya Baraza la Ulaya kuhusu Mahusiano ya Kigeni imeonya katika ripoti yake juu ya matokeo mabaya ya mashambulizi ya kijeshi wa Marekani nchini Iran.

Taasisi ya Ushauri ya Baraza la Ulaya imeonya kuhusu matokeo mabaya ya uingiliaji kati wa kijeshi wa Marekani nchini Iran na kutoa wito kwa serikali za nchi za Ulaya kufanya kazi na washirika wao wa kikanda ili kuzuia hatua yoyote ya kijeshi ya Washington.

Taasisi hiyo yenye makao yake makuu Berlin inaandika kwamba tangu mwaka 1979, marais wa Marekani wamekuwa wakikabiliwa na swali kwamba je, wanaweza kuiangusha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutumia nguvu za kijeshi?

Kufuatia machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, Rais Donald Trump wa Marekani alijitokeza hadharani na kutangaza akiwaambia maajenti wa Marekani na Israel waliohusika na uharibifu nchini Iran kwamba “msaada unakuja,” lakini lengo lake kuu bado halijabainika. Trump pia ametishia mara kwa mara kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran.

Taasisi ya Ushauri ya Baraza la Ulaya la Mahusiano ya Kigeni imeashiria uzoefu wa Afghanistan, Iraq, Libya na Syriana kusisitiza kwamba Marekani na Ulaya lazima ziwe na uhalisia kuhusu ufinyu wa ushawishi wa Magharibi na hatari za vita vya muda mrefu na Iran. Taasisi hiyo imeandika: Ikiwa Marekani itaanzisha mashambulizi makubwa kwa lengo la kuondoa madarakani utawala, Tehran inaweza kuzidisha gharama za kisiasa za hatua hiyo kwa Trump kwa kushambulia vikosi vya majeshi ya Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Jeshi la Iran pia lina uwezo wa kushambulia vituo vya mafuta vya kikanda na kuvuruga usafirishaji wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kitendo ambacho kinaweza kuzidisha kwa kasi bei za nishati na bidhaa duniani.

Iran pia ina uwezo wa kuamsha mtandao wa washirika wake wa kikanda kwa ajili ya mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya washirika wa Marekani, ikiwa ni pamoja na Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *