‎#HABARI: Mwili wa mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika umekutwa juu ya njia ya reli inayounganisha Mkoa wa Tabora na Kigoma, katika maeneo ya Kata ya Malolo, mkoani Tabora.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu huyo anadaiwa kufariki dunia baada ya kuigonga Treni usiku wa kuamkia leo, ambapo sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwa, mikono, miguu, zimeonekana zimekatikatika huku maini na sehemu ya mapafu yakikutwa nje ya mwili kutokana na athari za ajali hiyo.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefika eneo la tukio mapema asubuhi ya leo na kuchukua mwili wa marehemu baada ya taratibu za awali kufanyika, kisha kuusafirisha hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na njia ya reli wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa ajali katika maeneo hayo, wakiona kuna haja ya utolewaji wa elimu elimu ya tahadhari kwa wakazi wanaopakana miundombinu ya usafiri huo mkoani hapo.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *