#HABARI: Serikali imewataka wazalishaji na wabunifu wa teknolojia za nishati safi kuongeza juhudi katika kutengeneza bidhaa zinazomudu gharama za wananchi wengi ili kupanua matumizi yake nchi nzima.
Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia, Bw. Nolasco Mlay, ametoa wito huo jijini Arusha alipokua akikagua utekelezaji wa agizo linalozitaka taasisi zenye watu zaidi ya 100 kuachana na nishati isiyo rafiki kwa mazingira.
Katika ziara hiyo, Mlay alitembelea wadau mbalimbali wakiwemo SIDO na kampuni binafsi, akipongeza juhudi zao za kutengeneza majiko ya kisasa kwa ajili ya taasisi na kaya.
Alisisitiza kuwa Wizara ya Nishati imejipanga kuhakikisha ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekelezwa kikamilifu, kwa kuhimiza taasisi zote kushirikiana ili kurahisisha mchakato wa wananchi kuhamia kwenye nishati mbadala.
Lengo kuu la Serikali ni kufikia asilimia 80 ya Watanzania wanaotumia nishati safi ifikapo mwaka 2034, hatua itakayosaidia kulinda afya na mazingira.
Mlay amezikumbusha taasisi zilizokwishaweka miundombinu hiyo kutoirejea nishati chafu, bali kuendelea kuitumia kikamilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.