‎#HABARI: Mkoa wa Singida umezindua rasmi kampeni ya upandaji miti kimkoa katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Halima Dendego, huku ukihimiza wananchi kuachana na nishati chafu ya mkaa na kuni na kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia.

Afisa Kilimo wa Mkoa, Somboi Harold, amebainisha kuwa jitihada hizi zinaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda mazingira na afya za wananchi kutokana na madhara ya ukataji miti na moshi wa kuni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ametoa maelekezo kwa watendaji kusimamia zoezi la upandaji miti, huku Katibu wa CCM mkoani humo, Lucy Shee, akihamasisha wazazi kupanda mti kwa kila mtoto anayezaliwa kama mkakati wa kufikia malengo ya mazingira.

Huku wananchi wa Singida waliojitokeza katika zoezi hilo wameunga mkono kampeni hiyo wakiamini itasaidia kurejesha uoto wa asili na kuboresha hali ya hewa mkoani humo.


‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *