Iran imesema kuwa nchi za kikanda zinafanya juhudi za pamoja ili kuzuia vita kwa vile zinaelewa vyema kwamba hatua yoyote ya kijuba dhidi ya Tehran itakuwa na madhara makubwa kwa eneo zima.

“Tunaamini kuwa nchi za kanda hii zinatambua vyema kwamba ukosefu wa usalama katika eneo hili na tishio lolote dhidi ya Iran litakuwa na madhara na taathira ambazo zitawathiri pia wengine,” amesema Esmaeil Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alipozungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran. 

Ameongeza kuwa nchi za kanda hii zinafanya juhudi za pamoja ili kuzuia kuongezeka mivutano kwa sababu zinatambua hatari ya hatua yoyote ya uvamizi dhidi ya Iran. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezisihi nchi zote kuwa macho mkabala wa uvumi wa vyombo vya habari na utumiaji mbaya wa masuala ya kieneo ya upande wa tatu. 

Esmaeil Baqaei ameashiria mazungumzo kati ya Iran na nchi za kanda hii hasa Saudi Arabia na kuzitaka nchi zote za eneo hilo kuzingatia hali ya mambo. 

Baqaei amebainisha haya kufuatia hatua ya Marekani ya kujizatiti kijeshi katika eneo la Magharibi mwa Asia na katika Ghuba ya Uajemi kunakokwenda sambamba na vitisho vya Rais Donald Trump kushu hatua mpya za kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. 

Kwa upande wao viongozi wa Iran wameapa kuwa hatua yoyote ya uchokozi dhidi ya nchi hiyo itakabiliwa na jibu la haraka na kali.  

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Sayyid Ali Khamenei ametahadharisha kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran litasababisha vita katika eneo zima la Magharibi mwa Asia. 

“Wanapasa kujua kwamba kama mara hii wataanzisha vita basi vita hivyo vitakuwa vya eneo lote hili”, amesema Ayatullah Khamenei. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *