Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kimepongeza mahakama Kanda ya manyara kw namna ambavyo imekuwa ikitekeleza mahukum yake ya usikilizaji na utoaji wa maamuzi kwa haraka kwa mashauri yanayopelekwa mahakamani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya TLS mwenyekiti wa Chama hicho Thadey Lista ametolea mfano kupungua kwa kesi nyingi za ndoa kutokana na maamuzi ya haraka yanayotolewa kwa kusikilizwa mashauri hayo bila kuchelewa.
Lista ametoa kauli hiyo ya pongezi wakati akitoa taarifa ya chama hicho cha wanasheria kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini mkoani manyara.
(Feed generated with FetchRSS)