Waendesha mashtaka wamewafungulia mashtaka watu tisa kwa makosa ya ugaidi kuhusiana na moja ya mauaji mabaya zaidi yaliyojiri jimbo la Benue mnamo mwezi Juni mwaka jana. Mauaji hayo yalilenga pakubwai jamii ya Yelwata.

Watu wasiopungua 150 waliuawa kwa umati tarehe 13 Juni mwaka jana wakati watu waliokuwa wamejizatiti kwa silha aina la AK-47 walipovamia jamii ya watu wa Yelwata katika jimbo la Benue, katikati ya Nigeria. 

Siku hiyo watu waliokuwa na silaha walivamia na kuchoma nyumba na kuwaua raia ambapo baadhi yao waliteketezwa kwa moto wakiwa hai. Raia wengi wa jamii ya Yelwata walijeruhiwa katika hujuma hiyo.

Jana Jumatatu, Mahakama Kuu ya Shirikisho katika mji wa Abuja, Nigeria  iliwasilisha mashtaka 57 yanayohusiana na ugaidi dhidi ya watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo.

Mahakama imeeleza kuwa watu hao tisa wanaoongozwa na Ardo Lawal Mohammed Dono, walikutana mara kadhaa na kupanga mashambulizi hayo kwa miezi kadhaa, huku wakikusanya fedha na kuwaajiri wahalifu waliokuwa na silaha.

Upande wa waendesha mashtaka pia umedai kuwa watuhumiwa hao waliwaamuru viongozi wa jamii katika jimbo la Nasarawa wawapatie fedha; jimbo ambalo waliripotiwa kufanya mikutano yao ya kupanga mauaji ya umati. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *