Mwenyekiti wa Kampuni za Bakhresa, Mzee Said Salim Bakhresa, amepongeza kwa dhati mchango mkubwa wa Watanzania na wateja wake kwa kuendelea kumuunga mkono katika kila hatua ya safari yake ya kibiashara.

Amesema uaminifu, imani na mshikamano huo vimekuwa nguzo kuu zilizochochea ukuaji wa kampuni za Bakhresa, na kuziwezesha kupanua wigo wa uzalishaji, ajira na huduma kwa jamii ndani na nje ya nchi.

Kwa upande mwingine, Mzee Bakhresa ameishukuru Serikali kwa kuweka sera na mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji, yaliyowapa wawekezaji nafasi ya kuwekeza kwa uhakika na kwa maslahi mapana ya taifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *