Michuano mikubwa ya soka barani Afrika ya AFCON itafanyika katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki; Kenya Tanzania na Uganda.

Hata hivyo baadhi ya wadau walioshuhudia maandalizi na mafanikio ya michuano hiyo nchini Morocco mwezi uliopita hadi mwezi huu, wanasema mataifa hayo ya Afrika Mashariki yana kazi kubwa kuweza kukidhi matarajio ya wachezaji na mashabiki wa michuano hiyo kwa kiwango stahiki.

Licha ya kutoshinda Kombe la AFCON walipomenyana na Senegal katika mechi ya fainali, Morocco walidhihirisha kuwa waliwekeza ipasavyo katika maandalizi ya dimba hilo kama wenyeji.

Mashabiki na viongozi mbalimbali katika ulimwengu wa soka wamesifu sana viwango vya michuano hiyo iliyodumu mwezi mmoja katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.

Rais wa Shirikisho la Kandanda barani Afrika CAF Patrice Motsepe alielezea kuwa kila kitu kuanzia miundombinu hadi viwanja vya michezo vilikuwa vya hali ya juu ambayo haijashuhudiwa barani Afrika.

Ni kwa msingi  huu ndipo mwandishi habari mmoja kutoka Ivory Coast kwa jina  Mamadou Gaye ameibua mjadala mkubwa pale alipoelezea kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yaani Kenya Tanzania na Uganda hayana uwezo wa kuwa wenyeji wa dimba hilo ikilinganishwa na Morocco.

Mwandishi huyo amefahamisha kuwa Morocco imepandisha kabisa viwango vya maandalizi ya michuano hiyo nan chi hizo tatu haziwezi kukidhi matarajio ya wachezaji na mashabiki kama walivyoshuhudia Morocco.

Gaye ametoa mfano kwamba nchi hizo tatu hazina barabara nzuri zinazounganisha miundombinu hiyo kutoka nchi moja hadi nyengine na pia kwamba viwanja vya michezo na nyenzo kama hoteli hazina viwango stahiki.

AFCON 2027: Maendeleo ya uwanja wa michezo Arusha

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Hata hivyo rais wa CAF Motsepe amelezea kuwa na imani kwamba chini ya kauli mbiu yao ya “pamoja’ mataifa hayo matatu yataweza kuwa wenyeji stahiki wa michuano hiyo itakayofanyika mwaka ujao katikati.

Amesema kuwa ana wajibu wa kukuza soka barani Afrika na hawezi kuhamisha dimba hilo kutoka mataifa hayo. Kocha wa timu ya taifa ya Kenya Benni McCarthy ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini iliyoandaa kombe la dunia mwaka 2011, anakubaliana na rais wa CAF.

Itakumbukwa kwa mataifa hayo matatu yalikuwa wenyeji wa dimba la CHAN ambalo huhusisha wachezaji wa ndani ya nchi. Lakini michuano hilo iliahirishwa kutoka mwezi Februari hadi Agosti kwa sababu maandalizi yake yalikuwa bado ya kiwango cha chini.

Miongoni mwa changamoto zilizoibuka ni masuala ya uuzaji wa tiketi, udhibiti wa umati wa mashabiki ambao walivuka uzio wa usalama.

Wakati wa AFCON, rais wa CAF alielezea kuwa michuano ya CHAN ambayo imefanyikamara nane ingefutiliwa mbali kwa sababu ilileta hasara kubwa kifedha.

Hali ya uwenyeji pacha wa michuano ya AFCON kimataifa umewahi kuwepo mara mbili. Ghana na Nigeria walikuwa wenyeji wa michuano ya mwaka 2000 kisha Gabon na Guinea mwaka 2012.

Lakini hii ni mara ya kwanza kwa mataifa matatu kuwa wenyeji kwa pamoja. Hivi majuzi rais wa Uganda Yoweri Museveni alizindua moja kati ya viwanja vitakavyotumiwa kwa michuano hiyo Magharibi mwa nchi mjini Hoima. 

Kandanda | AFCON | Tanzania - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Yoane Wissa akipambana na wachezaji Bakari Mwamnyeto na Novatus Miroshi wa Taifa StarsPicha: Fadel SennaAFP/Getty Images

Kiwanja kimoja cha Kenya cha Raila Odinga Talanta kimeelezewa kuwa kwa kiwango cha asilimia 80 kukamilika, hii ni mwa mujibu wa taarifa za serikali ya nchi hiyo za wiki iliyopita.

Aidha hii itukuwa mara ya kwanza kwa mataifa yote 54 wanachama wa CAF kushiriki ambapo Eritrea imeahidi kuwa miongoni mwa timu washiriki.

Nchi hiyo iliyoshiriki mara ya mwisho miaka 19 iliyopita imesajili na hilo lilithibitishwa na rais wa shirikisho la Kitaifa la kandanda la Eritrea Paulos Andemariam alipohojiana na wanahabari Morocco mwezi uliopita.

Lakini maafisa wa Eritrea hawasemi waziwazi chanzo cha wao kutoshiriki katika kipindi hicho, suala hilo linanasibishwa na mienendo ya wachezaji wa timu ya taifa hiyo kutoweka na kujitambulisha kuwa waombaji hifadhi kutokana na ukandamizaji katika ambayo imetawaliwa na chama kimoja tu cha kisiasa tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka Ethiopia mwaka 1993 chini ya Rais Isaias Afwerki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *