Uhispania imekuwa nchi ya hivi karibuni barani Ulaya kuzingatia upigaji marufuku wa mitandao ya kijamii kwa watoto.
Waziri Mkuu Pedro Sanchez alitangaza hili katika hotuba yake Februari 3 huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Alisema serikali inapanga kuyataka majukwaa ya mitandao ya kijamii kuanzisha mifumo ya uthibitishaji wa umri na kupiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kutumia tovuti hizo.
Alionya kwamba watoto wanakabiliwa na unyanyasaji na vurugu, alisema: “Hatutakubali tena hili. Tutawalinda na ulimwengu wa kidijitali usio na sheria.”
Katika jibizo la wasiwasi unaoongezeka kuhusu athari hasi kwa watoto, Bunge la Ufaransa linajadili muswada ambao utapiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 15.
Serikali ya Denmark ilitangaza mnamo Novemba mwaka jana kwamba inapanga kuwazuia watoto walio chini ya umri wa miaka 15 kutumia mitandao ya kijamii.
Australia ilianza kutekeleza sheria inayopiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 mwezi Desemba mwaka jana, na kuwa nchi ya kwanza kuanzisha marufuku kulingana na umri.
Lakini changamoto zinabaki kama vile ni kwa jinsi gani majukwaa hayo yanavyoweza kuthibitisha umri wa watumiaji.