Katika jitihada za kuhakikisha vyanzo vya maji vinaendelea kuwa salama, Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu imewawezesha wananchi wa Kijiji cha Msonge, mkoani Morogoro, kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki.
Akizungumza katika zoezi la uvunaji wa samaki lililofanyika katika kijiji hicho, Afisa Kidakio cha Ruvu, Mhandisi Paschal Joseph amesema walianza na utoaji wa elimu kwa wananchi, kisha kuwasajili katika vikundi na kuwawezesha kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki, ili waachane na shughuli za uharibifu wa mazingira.
Paschal amesema lengo la mradi huo ni kuhusisha moja kwa moja jamii katika uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kuwapatia shughuli mbadala za kufanya pasipo kuathiri mazingira.
#AzamTVUpdates
✍Theresia Mwanga
Mhariri | John Mbalamwezi