Katika moja ya kambi kubwa za wakimbizi wa syria duniani Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kamishina Mkuu wa wakimbizi Salih amepata fursa ya kushuhudia kinachoendelea na mzigo wa wakimbizi unaobebwa na Jordan  

“Nipo hapa katika kambi ya wakimbizi ya Zaatari ambako Serikali ya Jordan ilipokea mawimbi ya kwanza ya wakimbizi wa Syria walipokuwa wakikimbia mauaji na machafuko nchini mwao, wakisaka usalama miaka 14 iliyopita.”

media:entermedia_image:b3d60238-bfe8-49bc-a63b-7f1aa97e3d1c

Adil Tughan

Kundi la wakimbizi kutoka Kambi ya Zaatari. (Maktaba)

Tangu wakati huo  ulipoanza mzozo wa Syria, Jordan imebeba mzigo mkubwa wa kuwahifadhi wakimbizi, ikiwapokea mamia ya maelfu licha ya changamoto za kiuchumi na kijamii zinazoongezeka. Salih ameipongeza Jordan kwa ukarimu wake wa muda mrefu, huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa 

Kwa miaka mingi, Jordan imewakaribisha kwa ukarimu mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Syria. Tunatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa michango yaokwa wakimbizi na Jorda kuhakikisha kwamba wakimbizi wanapewa wanachostahili.”  

Baada ya kuanguka kwa serikali ya Assad mwaka jana, matumaini yalifufuliwa kuwa uhamisho huu huenda ukafikia ukomo. Takribani wakimbizi wa Syria 180,000 tayari wameanza kurejea nyumbani kwa hiari kwa msaada wa UNHCR. Hata hivyo, wengi bado wana tahadhari.

Wakimbizi wengi niliokutana nao hapa leo wamesema hatimaye wanataka kurejea nyumbani, lakini wanataka kuhakikisha wako salama, wanaweza kupata riziki, kuwasomesha watoto wao na kupata huduma za msingi.”
Kwa sasa, karibu wakimbizi wa Syria 440,000 bado wanaishi Jordan na wanahitaji ulinzi na msaada unaoendelea. 

UNHCR inasema ufadhili endelevu ni muhimu si tu kusaidia wakimbizi walipo sasa, bali pia kuhakikisha kurejea kwao nyumbani kunakuwa kwa hiari, kwa usalama na kwa heshima.
Tangu mwaka 1950, UNHCR imekuwa ikilinda na kusaidia watu wanaokimbia vita na mateso na ili kuendelea na azma hii linahitaji msaada wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *