
Zaidi ya watu 1,000 wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao katika Kisiwa cha Panuitan kwenyemkoa wa Kaskazini wa Cagayan, kulingana na Wizara ya mambo ya ndani na serikali za mitaa.
Mamlaka ya hali ya hewa ya Ufilipino imesema kimbunga Ragasa kinachofahamika pia kwa jina la Nando kimeambatana na upepo wenye kasi ya kilometa 215 kwa saa.
Mamlaka hiyo imesema baadhi ya maeneo yanakabiliwa na hali inayotishia maisha na hakuna huduma ya umeme katika maeneo ya Pwani tangu Jumatatu asubuhi.