Utafiti huo wa kampuni ya Gallup umebainisha kuwa takriban asilimia 45 ya vijana nchini Marekani sasa wanajinasibu kama watu huru wasioshawishiwa na chama chochote cha siasa. Hayo ni mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, ambapo karibu theluthi moja ya Wamarekani walitaja kuwa hawajinasibishi na Wademocrats au Warepublican.
Kundi hili la vijana linaonekana kukua zaidi na linatokana na kukerwa kwao na hatua ziinazochukuliwa na chama kilichopo madarakani. Mabadiliko haya yanaweza kuwa na manufaa kwa chama cha Democratic katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwaka huu, lakini hilo halina uhakika hata kidogo.
Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana, wapiga kura wanaojinasibu kutoegemea upande wowote wameonekana wakivutiwa na chama cha Democratic lakini misimamo na mitazamo yao kuelekea chama hicho si ya kuaminika na huweza kubadilika.
Hilo linaonyesha kwamba mafanikio ya Wademokrasia labda yanahusiana zaidi na maoni ya watu huru kuhusu Rais Donald Trump yanayozidi kuwa mabaya. Hilo linaonyesha kwamba mafanikio ya Wademocrats huenda yametokana na mitazamo hasi ya vijana hao dhidi ya Rais Donald Trump.
Vijana wa sasa wanaonekana kuvitupilia mbali vyama vya siasa kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko vizazi vilivyopita. Zaidi ya nusu ya Kizazi cha GenZ na kile cha Millennials kilichozaliwa kati ya mwaka 1981 na 2007, hujinasibu kama watu huru wasio na msimamo wowote wa kisiasa, huku vizazi vingine vikionekana japo kukiunga mkono chama kimoja cha siasa, iwe Democratic au Republican.
Hali hii inaashiria mabadiliko ya mara kwa mara na makubwa yanayoshuhudiwa katika siasa za Marekani na huenda matukio kama hayo yakashuhudiwa mara kadhaa. Kwa muda mrefu, Wademocrats wamekuwa wakiwavuta zaidi vijana hao wanaojinasibu kuwa huru kisiasa ambao pia idadi yao imekuwa ikizidi kuongezeka katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Takriban asilimia 47 ya watu wazima nchini Marekani wanajinasibu kuwa Wademocrats huku asilimia 42 tu wakiwa ni Warepublican. Hii ikiashiria mitazamo ya kisiasa ya Wamarekani, jambo ambalo hata hivyo huenda lisidhihirike wazi katika daftari la wapiga kura.
Hata hivyo, wakati wa utawala wa Rais Joe Biden, Wademocrats walirejea katika nafasi waliokuwepo wakati wa muhula wa kwanza wa Trump. Hii si tu habari mbaya kwa chama hicho ambacho kinatarajia kujishindia ushawishi wa Baraza la Congress la Marekani mwezi Novemba, kwa kutegemea zaidi chuki ya vijana kwa Trump kuliko imani yao isiyoyumba kwa chama hicho cha Democratic. Umaarufu wa Trump miongoni mwa vijana hao umepungua kwa kasi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Utafiti huu wa Gallup umeweka bayana kuwa mwelekeo huu wa vijana kutojinasibisha na chama chochote cha siasa huko Marekani na kujitambulisha kama “huru” hautabadilika katika kipindi cha hivi karibuni isipokuwa wadau mbalimbali wa siasa waweze kubadili mtazamo wao kwa vijana kwa kuchukua hatua stahiki.
