Hali ya huzuni na simanzi imetanda miongoni mwa wakazi wa mtaa wa Kitwiru, Manispaa ya Iringa, kufuatia kifo cha mtoto Geofrey Malate (11), aliyefariki dunia baada ya kuzama katika Mto Ruaha Mdogo.
Inaripotiwa kuwa Geofrey, aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Kilonga A, alipata ajali hiyo wakati akijaribu kuogelea katika mto huo, lakini alishindwa kumudu kasi ya maji na hatimaye kuzama, hali iliyosababisha kifo chake.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi