Halmashauri ya Wilaya ya Ilala imetenga Shilingi Bilioni 14 kutoka katika makusanyo ya ndani kwa ajili ya kuboresha miundombinu mbalimbali wilayani humo ikiwemo barabara.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alisema hatua hiyo inaakisi maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuongeza utegemezi wa mapato ya ndani katika kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kutegemea wafadhili.��
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa mita 400, Mpogolo amesema ukuaji wa makusanyo ya Halmashauri unaipa fursa ya kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya barabara.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)