Mpango huu ni utekelezaji wa agizo la Nchi Wanachama kupitia Mkataba wa Zama Zijazo, unaolenga kuimarisha suluhu za kimataifa kuhusu teknolojia mpya zinazoathiri kila nyanja ya maisha.

Jopo hilo litakuwa chombo cha kwanza cha kisayansi cha kimataifa kilicho huru kikamilifu, chenye lengo la kutathmini athari halisi za AI katika uchumi na jamii, pamoja na kusaidia kuziba pengo la maarifa kuhusu teknolojia hii.

Ushirikiano

“AI inasonga kwa kasi ya mwanga,” amesema Guterres, akisisitiza kuwa hakuna nchi inayoweza kuona picha kamili peke yake. Amebainisha umuhimu wa kuwa na uelewa wa pamoja ili kujenga mifumo madhubuti ya udhibiti, kuendeleza ubunifu kwa manufaa ya wote, na kukuza ushirikiano wa kimataifa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, jopo hilo litakuwa rejea ya kuaminika, likisaidia kutofautisha sayansi sahihi na taarifa potofu, katika wakati ambao uelewa wa kweli na usioegemea upande wowote kuhusu AI ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Wajumbe waliopendekezwa walichaguliwa baada ya wito wa wazi wa kimataifa uliopokea zaidi ya maombi 2,600. Orodha ya mwisho inajumuisha wataalamu wa fani mbalimbali, ikiwemo ujifunzaji wa mashine, usimamizi wa data, afya ya umma, usalama wa mtandao, maendeleo ya mtoto, na haki za binadamu. Wajumbe wote watahudumu kwa uwezo wao binafsi, bila kuwakilisha serikali, kampuni, au taasisi yoyote.

Matarajio

Inatarajiwa kwamba jopo hilo litaanza kazi mara moja, huku ripoti yake ya kwanza ikipangwa kuwasilishwa kwa ajili ya kuchangia Mazungumzo ya Kimataifa kuhusu Utawala wa AI yatakayofanyika mwezi Julai.

Guterres amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja, akisema kuwa akili mnemba inaibadilisha dunia kwa kasi. Ameonya kuwa changamoto kuu ni iwapo mataifa yataunda mwelekeo wa mabadiliko haya kwa pamoja, au yataacha teknolojia hiyo ijiendeshe yenyewe bila usimamizi wa pamoja  hasa katika kipindi hiki cha mvutano wa kisiasa duniani na ushindani unaoongezeka wa kiteknolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *