Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani mashambulizi makubwa ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza yaliyouwa shahidi Wapalestina 23 tangu ustishaji vita wa Oktoba mwaka jana na ksuema kuwa hujuma hiyo ya utawala wa Kizayuni inathibitisha kuwa namna Israel inavyoendeleza kampeni yake ya mauaji ya kimbari.

“Kuendelea  mashambulizi ya Israel kunadhiirisha nia ya makusudi ya mhalifu wa kivita Netanyahu ya kuhujumu awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano, hasa kuhusiana na kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah,” imebainisha taarifa ya Hamas.

Wakati huo huo Hamas imekadhibisha madai ya Israel kuhusu tukio la ufyatuaji risasi  lililolenga mmoja wa askari wake kaskazini mwa Gaza. Hamas imesema kuwa madai haya ya Israel ni visingizio dhaifu kwa lengo la kuhalalisha mauaji yake ya kimbari inayoyaendeleza dhidi ya wananchi wa Palestina na ni jitihada za utawala huo ghasibu za kulitwisha eneo la Gaza hali ya ukandamizaji na hofu ya kudumu. 

Harakat hiyo ya mapambno ya ukombozi ya Palestina imewatolewa wito wafadhili na wapatanishi wa makubaliano ya kusitisha mapigano kupinga vikali hatua za mhalifu wa kivita Netanyahu.

Hamas imesisitiza kuwa kuwa Waziri Mkuu wa Israel kwa makusudi anajaribu kuhujumu makubaliano ya kusitisha mapigano ili kuanzisha tena kampeni ya mauaji na njaa huko Gaza.

Duru za tiba zimearifu kuwa watoto kadhaa ni miongoni mwa Wapalestina waliouliwa shahidi juzi Jumatano akiwemo binti aliyekuwa na umri wa miaka 11. 

Takriban watu 14 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel katika vitongoji vya Tuffah na Zeitoun katika mji wa Gaza. Wengine wanne waliuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni shambulizi dhidi ya makazi ya wakimbizi wa KIpalestina katika eneo la Qizan Abu Rashwan, kusini mwa Khan Younis, kusini mwa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *