Ofisi ya Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imejibu kuhusu kufutwa kwa vyama vya siasa nchini Burkina Faso, uamuzi uliofanywa na utawala wa kijeshi unaotawala. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ametaka “nafasi halisi ya kiraia na kidemokrasia” nchini Burkina Faso.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hii si hatua katika mwelekeo sahihi kwa haki za binadamu za raia wa Burkina Faso,” alisema Kamishna Mkuu Volker Turk kuhusu kufutwa kwa vyama vya siasa, hatua iliyotangazwa na utawala wa kijeshi mnamo Januari 29.

Kamishna Mkuu, ambaye wakati wa ziara yake ya mwisho Ouagadougou mnamo mwezi Juni 2024 alitoa wito wa uchunguzi kuhusu mauaji ya raia—uchunguzi ambao haujawahi kufanyika—sasa ana wasiwasi, mwaka mmoja na nusu baadaye, kuhusu kufutwa kwa vyama vya siasa na utawala wa kijeshi. Utawala wa kijeshi ambao hauheshimu tena maamuzi ya mahakama, unakandamiza uhuru wa vyama vya wafanyakazi, na unawakamata kikatili wapinzani na wakosoaji.

Katika muktadha huu wa sera za ukandamizaji za Burkina Faso, Kamishna Mkuu Turk alisema kwamba “badala ya kupiga marufuku vyama vya siasa na kuwafunga watu” wanaotoa maoni yao, “mamlaka za Burkina Faso zinapaswa kufungua nafasi kwa mashirika ya kiraia, kuheshimu uhuru wa kujieleza, na kuondoa marufuku ya shughuli za vyama vya siasa.”

Ili kutimiza matakwa haya yeye manufa kwa wote, shirika hili la Umoja wa Mataifa linataja kile walichokubaliana na Ouagadougou, ambayo, kulingana na Volker Turk,  itaiwajibisha serikali ya Burkina Faso. Ahadi kuhusu uhuru wa msingi zilipatikana mnamo mwezi Desemba 2025, lakini athari zake halisi ni ngumu kupima, kamata kamata na visa vya utekaji nyara kiholela viliongezeka mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *