Nchini Niger, kuna shambulio lilitokea katika mkoa wa Tillabéri siku ya Jumatano, Februari 4. Washambuliaji walilenga kambi ya vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger huko Makalondi, kilomita 90 kutoka Niamey. Shambulio hilo limedaiwa na JNIM, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu. Kulingana na vyanzo vya usalama, afisa wa polisi aliuawa na magaidi hao, lakini hakuna idadi rasmi ya vifo iliyotangazwa. Hii si mara ya kwanza eneo hili karibu na Burkina Faso kulengwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea alasiri. “Watu walikuwa wakijiandaa kwa sala walipoanza kusikia milio ya risasi,” chanzo cha ndani kimesema.

Washambuliaji walishambulia kambi ya pamoja ya vikosi maalum vya Niger na kampuni inayosimamia mipaka. Walichukua udhibiti baada ya wanajeshi kuondoka na kuchukuwa vifaa. Kulingana na vyanzo vya usalama, afisa wa polisi aliuawa. Jenerali Salaou Barmou, Mkuu wa majeshi ya Niger, alizuru eneo hilo sku ya Alhamisi.

Mbali na ngome ya vikosi vya FDS, hakujathibitishwa uharibifu wowote ulioweza kutokea katika eneo hilo. Watu kadhaa waliowasiliana nao hawajafika kattika kambi hiyo tangu wakati huo. Mji huo, ambapo shule zimefungwa, umeshuhudia watu wengi wakihama makazi yao.

Miezi michache iliyopita, wakazi wa Makalondi walielezea wasiwasi kuhusu shinikizo kutoka kwa makundi yenye silaha. Mwalimu alitekwa nyara katika mji huo mnamo mwezi Desemba. Mwezi uliopita, gavana wa Torodi, mji ulioko kilomita 60 kutoka Niamey, aliuawa nyumbani kwake pamoja na familia yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *