Kutokana na sera ngumu za biashara za Marekani, Pretoria inaharakisha mpango wake kuelekea Beijing. Afrika Kusini inajiandaa kusaini makubaliano na China kutoa ufikiaji usiotozwa ushuru kwa baadhi ya bidhaa zake za nje, katika mkakati wa makusudi wa mseto wa soko.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu nchini China, Clea Broadhurst

Kwa kutoa uagizaji usiotozwa ushuru wa baadi ya bidhaa za Afrika Kusini, Beijing inaimarisha uhusiano wake na mshirika wake mkubwa wa biashara wa Afrika na kujiweka kama bingwa wa biashara huria wakati wa kuibuka tena kwa ulinzi wa Magharibi.

Ingawa Marekani imeweka ushuru wa 30% kwa baadhi ya bidhaa za nje za Afrika Kusini, China inakuza ushirikiano wa “nufaika kwa wote”, ikichanganya biashara na uwekezaji.

Ziara ya Waziri wa Biashara wa Afrika Kusini kwenda Beijing pia inatarajiwa kuwezesha mikutano na kampuni za China zinazopenda sekta za madini, kilimo, na viwanda. Kwa mamlaka ya China, ushirikiano huu unaonyesha nia yao ya kuimarisha ushawishi wao wa kiuchumi barani Afrika huku ikihakikisha usambazaji wao wa madini ya kimkakati na bidhaa za kilimo.

Pia inatuma ujumbe ulio wazi wa kisiasa: Pretoria inarekebisha usawa wake wa diplomasia ya kiuchumi, ikitegemea Asia kupunguza misukosuko ya ng’ambo ya Atlantiki na kuhakikisha ukuaji wake. Katika muktadha huu, Beijing inakusudia kujionyesha kama nguzo ya utulivu wa biashara na mshirika wa kuaminika kwa uchumi unaoibuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *