Rais wa Marekani Donald Trump anasema atafanya mkutano na Waziri Mkuu wa Japani Takaichi Sanae jijini Washington mwezi ujao.
Trump alisema kwenye mitandao ya kijamii Februari 5 kwamba, “Ninatazamia kumkaribisha Waziri Mkuu Takaichi katika Ikulu ya Marekani Machi 19.”
Akizungumzia ziara yake nchini Japani mwaka jana, Trump alisema alivutiwa sana na Takaichi.
Aliongeza kuwa Marekani na Japani zimefanya kazi kwa karibu katika usalama wa taifa, pamoja na kile anachokiita “Makubaliano ya Biashara” muhimu sana yanayozinufaisha zaidi nchi zote mbili.
Trump pia alizungumzia uchaguzi wa Baraza la Chini la Bunge la Japani uliopangwa kufanyika Februari 8.
Aliandika kwamba, “kama Rais wa Marekani, ni Heshima kwangu kumpa Idhinisho Kamili na Lote.”
Trump awali ameonyesha kuunga mkono wagombea katika chaguzi zinazofanyika nje ya Marekani. Lakini ni nadra kwa Rais wa Marekani kutangaza msimamo wake kuhusu uchaguzi nchini Japani.