Akizungumza jana katika hafla moja iliyofanyika katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, Kagame alionekana kujibu maswali kwa kusisitiza uhuru wa nchi hiyo.

” Kiwango cha vitisho tunavyokabiliana navyo kila siku. “Yaani, Tutafanya hivi usipofanya hivi, tutafanya vile usipofanya vile,” unajua. Wakati mwingine unahisi kusongwa na vitisho vya aina hii ya lakini badala ya kusongwa na hayo yote, nitasongwa na kukaidi na kukuambia potelea mbali.”

Rwanda inasisitiza kuwa inahusika tu mashariki mwa Kongo ili kujilinda dhidi ya kundi la wanamgambo lililoundwa kutoka kwa wahusika waliobaki wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, na kukanusha kuhusika moja kwa moja kijeshi licha ya ushahidi mkubwa kutoka kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *