KUTOKA KWA ‘MADIBA”: Mtanzania Jackson Ng’anyi ametinganusu fainali ya mashindano ya mchezo wa Pool kwa kumfunga Mtanzania mwenzke Omary Akida hatua ya robo fainali.
Katika mchezo huo, wachezaji wote walionesha kiwango kizuri na kuufanya mchezo huo kufika fremu 6-6 na hatimae bingwa akapatikana kwa kupiga penati.
Baada ya kusonga mbele, sasa Jackson atakutana na Harry Martin wa Afrika Kusini saa nane mchana kuitafuta tiketi ya kucheza fainali.
Katika michezo mingine ya robo fainali Mtanzania Melckzedeck amadeus amepoteza kwa fremu 7-6 dhidi ha Mzambia Latham Kaunda.
Kwa upande wa Wanawake Cecilia kileo amepata ushindi wa fremu 4-2 dhidi ya Doreen Wandia wa Kenya.
Michezo ya nusu fainali kwa wanawake itachezwa leo Februari 6, saa moja usiku.
#PoolTable #Pool